Mwanamitindo wa kiume toka Brazil mwenye miaka 26 amefariki dunia alipokua akifanya onyesho la mavazi katika tamasha la mitindo la São Paulo.

Tales Soares ameripotiwa kuanguka baada ya kutegwa na kamba za viatu alivyokuwa amevaa.

Mtayarishaji wa onesho hilo la mitindo la Sao Paolo hajataja chanzo hasa cha kifo cha mwanamitindo huyo kilichotokea gafla akiwa stejini.

Kupitia ukurasa wake wa instagram mtayarishaji wa onesha hilo ameandika kama kumbukumbu ya mwanamitindo huyo amesema.

”SPFW imepokea taarifa juu ya kifo cha mwanamitindo Tales Soares ambaye aliumwa gafla kwenye maonesho ya mitindo ya Ocksa”.

Waliohudhuria tamasha hilo awali walifikiri kuanguka kwake kulikua sehemu ya onyesho lake lakini walishtukia amebebwa kutoka ukumbini hapo na walinda usalama akiwa ameziraia.

Ambapo alikimbizwa hospitali, bahati mbaya madktari hawakuweza kuyaokoa maisha yake.

Kanda za video zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zimemuonesha Soares akitembea kwa mwendo wa madaha kisha akageuka na kuangalia nyuma kabla ya kuanguka chini lakini picha hizo hazikutolewa maelezo yoyote.

Aidha, Salamu za pole zimetumwa kwa ndugu wa karibu kw akupotezewa na mpendwa wao Mwanamitindo Tales Soares.

Sir Lanka yapiga marufuku mavazi ya Nikabu kwa wanawake
Benin yafanya uchaguzi bila wagombea wa Upinzani

Comments

comments