Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hasna Attai Masoud amekuwa mwanamke wa pili kujitokeza kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea urais visiwani Zanzibar.

Hasna anafanya idadi ya watia nia kupitia Chama cha Mapinduzi hadi sasa kufikia 25 visiwani humo.

Mwantum Mussa Sultan alikuwa Mwanamke wa kwanza kuchukua fomu ya Urais kwa tiketi ya CCM na na Mwanachama wa 11 kujitokeza.

Wengine waliochukua fomu ni Mbwana Bakari Juma, Ali Abeid Karume, Hamad Massauni, Mbwana Yahya Mwinyi, Dkt. Hussein Mwinyi, Omar Sheha Mussa, Shamsi Vuai Nahodha, Mohamed Hija Mohammed, Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Salum Hashim Salum, Mohammed Jaffar Jumanne na Balozi Meja Jenerali Mstaafu Issa Suleimani Nassor.

Zoezi la utoaji fomu linaendelea katika Ofisi Kuu za CCM zilizopo Kisiwandui na linatarajiwa kukamilika Juni 30,2020.

Kamati ya nidhamu TFF yawahukumu Morrison, Mkude
IGP: Mbowe atashtakiwa ikibainika alidanganya shambulio