Mwanamuziki wa Marekani, Christina Grimmie ameuawa kwa kupigwa risasi katika tamasha lake ililofanyika Orlando, Florida nchini humo.

Mwakilishi wa mwimbaji huyo, jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa Grimmie ambaye aliwahi hushiriki mashindano ya kuimba ya ‘The Voice’ alipigwa risasi kadhaa na mtu ambaye hajafahamika, na alifariki akiwa umri wa miaka 22.

“Tunaomba katika kipindi hiki kigumu, watu waheshimu faragha ya familia yake na marafiki wa karibu wanapoomboleza kifo cha mpendwa wao,” alisema mwakilishi huyo.

Kitengo cha Polisi cha Orlando kimetoa taarifa rasmi ya kuthibitisha tukio hilo. Taarifa hiyo imeeleza kuwa Grimmie alimaliza tamasha majira ya saa nne usiku na kusubiri kusaini (autograph) za mashabiki wake, lakini alitokea mtu asiyejulikana na kumpiga risasi.

Imeeleza kuwa kaka yake Grimme alijaribu kumdhibiti mtu huyo ili asilete madhara kwa watu wengi zaidi lakini baada ya kuona anazidiwa alijipiga risasi na kufariki papohapo.

Kangi Loguola alia na Kodi kwa Wabunge, adai watarudi kuwa ombaomba
Wabunge Ukawa 'wajiengua' baada ya Ikulu kuwazuia kwenda Marekani na kumruhusu wa CCM