Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ametembelea na kusikiliza kero zinazowasumbua wananchi wa Kilosa ambapo kumekuwa kukitokea ugomvi wa mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji.

Aidha, Mwigulu amesema kuanzia sasa likitokea tukio lolote la watu kuuana kwa mapanga, mikuki, sime  na silaha zozote za jadi zinazotumiwa hasa na wakulima na wafugaji, Serikali itafuta utaratibu wa kubeba silaha hizo na atakayebeba atakamatwa na kuchukuliwa hatua kama watuhumiwa wengine.

Hata hivyo, Mwigulu amewaagiza wakulima na wafugaji kwa pamoja kuwakamata watu wote watakaohusika na kuanzisha vurugu na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola kabla ya Jeshi la Polisi halijafanya maamuzi yake.

“Kuanzia leo tunaanza kuhesabu pakitokea tukio lolote la vurugu na zikatumika silaha kuwadhuru wananchi, tutafuta utaratibu wa watu kutembea na silaha mitaani, na ukikutwa nayo unakamatwa kama ambavyo mtu mwenye silaha ya moto. Hatuwezi kuruhusu hii ikawa nchi ya watu wanakatana katana tu,”amesema Nchemba.

Zitto: Hali ya chakula nchini ni mbaya
UVCCM waunga mkono kutumbuliwa kwa Mramba