Saa chache baada ya Kuapishwa na Rais John Magufuli kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba jana aliwatangazia kiama wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwigulu alisema kuwa atawashughulikia wafanyabiashara wa dawa za kulevya na kuwashauri watafute kazi nyingine ya kufanya kuanzia muda huo.

“Wanaofanya biashara ya dawa za kulevya ni bora wakaacha, nawashauri watafute kazi nyingine ya kufanya,” alisema Nchemba.

Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa miongoni mwa makada wa CCM waliochukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi chama hicho, juzi alihamishwa kutoka kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuziba pengo lililoachwa na Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake uliteuliwa.

Video: 'Lipumba aomba cheo chake CUF, Zitto atoa mazito kwa JPM' - Magazeti
Naibu Spika avunja rekodi, Aanza kujitetea Asing'olewe