Uchunguzi wa awali unaoendelea kufanywa na serikali ya nchini Uswiz kufuatia sakata la ufisadi lililojikiota kwenye shirikisho la soka duniani FIFA, umebaini kulikua na mgongano wa kimaslahi kati ya rais Sepp Blatter dhidi ya rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini.

Mwenyekiti wa ofisi wa mkaguzi wa hesabu za serikali wa nchini Uswiz, Domenico Scala, amesema jambo hilo limebainika kutokana na shughuli za kiuchunguzi zinazoendelea kufanywa kwenye ofisi za FIFA kwa sasa.

Scala, amesema malipo yanayodaiwa kufanywa dhidi ya rais wa UEFA Michel Paltini, hayajawekwa kwenye rekodi za FIFA, hatua ambayo inaendelea kudhihirisha kulikua na njia za mkato za mgongano wa kimaslahi kwa viongozi hao wawili.

Amesema katika utaratibu wa kawaida, malipo hayo yalitakia kufanya na kuweka kwenye kumbu kumbu za FIFA ili kudhihirisha ukweli wa jambo hilo kufanyika kihalali, hivyo kutokana na waliyoyaona wameendelea kuamini kulikua na mchezo mchafu.

Hata hivyo, Scala amedai kwamba uchunguzi unaendelea kufanyika na wanaamini huenda kuna mambo mengine yaliyokua yamefikika kwa maslahi ya wachache kwenye ofisi za FIFA wakayabaini.

Blatter, mwenye umri wa miaka 79, anadaiwa aliidhinisha malipo ya paund million 1.35, ambayo yalienda kwa rais wa UEFA Platini, mwenye umri wa miaka 60, mwaka 2011.

Wawili hao wanaendelea kutumikia adhabu ya kufungiwa kwa siku 90, kujihusisha na masuala ya soka, ambayo ilitolewa mwanzoni mwa mwezi huu na kamati ya maadili ya FIFA, ili kupisha uchunguzi dhidi yao kufanywa na serikali ya nchini Uswiz.

Guardiola: Sina Desturi Ya Kumlaumu Mchezaji
Eminike Amfuata Enyeama Kwa Maamuzi Binafsi