Beki na nahodha wa kikosi cha Man City Vincent Jean Mpoy Kompany atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma saba, baada ya kupata majeraha ya goti katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Crystal Palace waliokubali kucharazwa bakora mbili kwa moja (2-1).

Meneja wa Man city Pep Guardiola, amethibitisha taarifa za beki huyo kutoka nchini Ubelgiji alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kikosi chake kuelekea kwenye mpambano wa mzunguuko wa tano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Borussia Moenchengladbach.

Kompany alipatwa na majeraha ya goti akiwa amerejea katika kikosi cha Man city kwa mara ya kwanza baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi saba, lakini kwa bahati mbaya ilipofika dakika ya 37 ya mchezo dhidi ya Crystal Palace, aligongana na mlinda mlango wake Claudio Bravo.

“Ana matatizo ya goti. Anaweza kukaa nje ya uwanja kwa majuma kadhaa yajayo,” Guardiola aliwaambia waandishi wa habari.

“Amekua na majonzi makubwa sana kufuatia majeraha hayo. Kwa sasa yupo safarini nchini Hispania kwa ajili ya kufanyiwa matibabu na nina matumaini atapona katika muda muafaka.” Aliongeza Guardiola

Endapo Man City watafanikiwa kuchomoza na ushidni hii leo watakua wamefaulu kutinga kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Gareth Bale Amtia Mshawasha Zinedine Zidane
Serge Aurier Apigwa Stop Kuingia London