Rafael Nadal, raia wa Hispania ametangaza kujiondoa katika michuano ya wazi ya Mexico baada kutonesha jeraha lake la paja ambalo lilimsababishia ajitoe kwenye michuano ya Australia.

Nyota huyo namba mbili kwa ubora wa tennis duniani, alikuwa tayari amepangwa kucheza dhidi ya Mhispania mwenzake Feliciano Lopez katika hatua ya ufunguzi mjini Acapulco nchini Mexico.

“Hapo jana wakati wa mazoezi nilihisi kuna kitu kinanighasi, nikalazimika kwenda hospitali kujitazama na kufanya kipimo cha MRI na bado nalazimika kufanya vipimo vingine zaidi kujua nini hasa kinaendelea, lakini ni sehemu ile ile iliyonifanya nisishiriki michuano ya wazi ya Australia,” amesema Nadal.

Kuhusu mashindano ya Indian Wells, Nadal amesema hana uhakika kama atakuwa amepona, lakini atahakikisha anakwenda kushiriki.

“Ntafanya kila namna niweze kwenda ingawa siwezi kukubali au kukataa kama nitakwenda, natumai nitapata majibu mazuri, na baadaye tutajua itakavyokuwa,” amesisitiza Nadal.

Pochettino aupinga mfumo wa uamuzi wa kutumia video
Athuman Bilal: Simba ni timu ya kawaida