Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Nassor Ahmed Mazrui ambaye jana alihojiwa kwa muda wa zaidi ya saa tatu na nusu katika makao makuu ya Jeshi la Polisi Mjini Unguja ameeleza alichoelezwa na jeshi hilo.
Mazrui aliwasili katika makao makuu ya Chama chake na kulakiwa na mamia ya wafuasi wa chama hicho, muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamani iliyokuwa na masharti ya kuwasilisha wadhamini wawili ambao walitoa kiasi cha shilingi 500,000 kila mmoja.
Alisema kuwa polisi walimtuhumu kwa uchochezi kufuatia maneno yake aliyoyatoa katika moja ya mikutano ya hadhara ya chama hicho hivi karibuni, kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana ambao chama hicho kinadai kuwa kilishinda, na kutangazwa kwa uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu.