Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amekipongeza chama cha NCCR Mageuzi kwa kuendelea kutii sheria na matakwa ya nchi na kuachana na ile tabia ya wapinzani wanaoendekeza chuki, bugudha, matusi pamoja na masuala yanayoleta mitafaruku katika nchi.

Ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa kuchagua viongozi wa chama hicho, ambapo amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Magufuli inachukizwa na wapinzani wasiofuata kanuni na taratibu za nchi.

”Serikali ya Awamu ya Tano haichukii upinzani ila inachopingana nacho ni wapinzani na mpinzani ni yule anayefuata sheria na kanuni na anayesimamia maadili ya nchi kama huyu James Mbatia na ni M/kiti wa chama cha upinzani na sio wapinzani, ameweka pembeni chuki, bughudha, matusi na kila jambo linaloleta mtafaruku,”amesema Nyahoza.

Aidha, Nyahoza amesema kuwa yeye kama Naibu msajili, anakiona chama cha NCCR Mageuzi ndio chama cha kuigwa na vyama vingine na kwamba anaiona safari nzuri ya chama hicho.

”Chama cha NCCR Mageuzi ni chama cha mageuzi kwa sababu mumeendelea kutii sheria za nchi kama zinavyoelekezwa hii inathibitisha kwamba nyinyi ni baba wa mageuzi na mimi kama Naibu msajili wa vyama, naunga mkono kabisa mwenendo wa NSSR Mgeuzi katika nchi hii,”Ameongeza Nyahoza

Mbegu feki zamponza mfanyabiashara
Lazima kuna walimu wamejazana pale Ruangwa Mjini, wahamisheni- Majaliwa