Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Mbozi, John Palingo kumkamata mfanyabiashara aliyewauzia wakulima mbegu feki katika wilaya hiyo na kupelekea kuathiri mavuno kwa wakulima.

Ametoa agizo hilo kufuatia swali la mkulima mmoja mkazi wa Kijiji cha Malolo, Isaya Nyondo ambaye alitaka kujua hatua zipi zinachukuliwa na serikali kufuatia kuuziwa mbegu feki na hivyo kufanya washindwe kuvuna mwaka huu.

“Katika hili namuagiza Mkuu wa Wilaya kumkamata msambazaji wa mbegu hizo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa,” amesema waziri Hasunga.

Hasunga amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli imekusudia kuimarisha Sekta ya Kilimo hivyo mfanyabiashara yeyote anayecheza na ufanisi wa wakulima atachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Ujumbe wa IGP Sirro kuhusu mali za askari
Naibu Msajili wa vyama vya siasa akisifia chama cha NCCR- Mageuzi