Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Posta na Mawasiliano wa nchi hiyo, Enock Ruberangabo Sebineza aliyenaswa akijichua (punyeto) ofisini kwake.

Utenguzi huo umekuja baada ya kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii kipande cha video kinachomuonesha naibu waziri huyo akijichua ofisini kwake.

Kwa mujibu wa Televisheni ya Taifa ya Congo, Rais Kabila amelaani kitendo hicho na kudai kuwa kigogo huyo ameiaibisha nchi hiyo.

Video ya tukio hilo la aibu ilisambaa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mitandao ya kijamii huku bendera ya nchi hiyo na picha ya Rais Kabila vikionekana nyuma yake.

Hukumu Ya Bocco, Tambwe, Ngoma Kufahamika Kesho
Rais wa Korea Kaskazini apiga marufuku Ndoa na Misiba