Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara, awataka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kutazama upya kipengele cha malipo kwa Mkandarasi M/S Xiamen Ongoing Construction Group Company Limited anayejenga Bandari ya Karema ili kutomchelewesha kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Ametoa kauli hiyo Mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bandari hiyo ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 72.

Ujenzi wa Bandari hiyo unahusisha ujenzi wa kidhibiti mawimbi,maegesho ya meli,eneo la kuhudumia meli,jengo la abiria,ofisi za wadau wa Bandari,ghala la kuhifadhia mizigo,ukuta, yadi ya kuhifadhia mizigo mchanganyiko na makasha na ujenzi wa miundombinu ya maji,umeme,usalama na tehama.

Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi march 2022 na umegharimu zaidi ya Tsh billion 45.

Maamuzi Ligi Kuu England kujulikana leo
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Disemba 20, 2021