Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu amemuomba Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere kutembelea miradi ya maji iliyopo kwenye wilaya hiyo ili awezekuwa huru katika uongozi wake.

Akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha bodi ya barabara ya mkoa wa Mwanza kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Tabasamu amesema miradi ya Maji bado ina ubabaishaji kwenye jimbo hilo.

Tabasamu amesema kuna miradi mingi ya maji ukiwamo wa Nyamazugo ambao umegharimu Sh. Bilioni 23 na mpaka sasa haujakamilika takribani miaka mitatu.

“Miradi ya maji iliyopo Sengerema ni ya ujambazi tumezungumza na CAG na watu wake na leo hii nimezungumza na kwenye kikao hiki tumekubaliana na Suwasa, Mwauwasa na Ruwasa tunataka  tuirudie kuikagua kwani inatesa wananchi wakisikia Sh. Bilioni 1.3 na Bilioni 1.6 alafu hakuna maji wanaumia sana,” ameongeza Tabasamu.

“Sengerema kuna mradi wa Busubwangili wa Sh. Milioni 400 wa Katungulu-Nyamtelela wa Sh milioni 730, Chabanda-Kasingamile wa Sh. Bilioni 1.35 yaani hadi kichefu chefu kutaja  ee…Mungu wee naomba CAG aje haraka ili niwe huru katika uongozi wangu,” amesema Tabasamu.

Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi
Mkuchika: Watendeeni haki wanaoomba ajira

Comments

comments