Serikali ya awamu ya Tano imewahakikishia waandishi wa habari neema ya maslahi, usalama na uhuru wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa maslahi mapana ya Taifa.

Hayo yamesemwa juzi na Waziri wa Habara, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alipokuwa akizungumzia siku 100 za Rais Magufuli kupitia kituo cha runinga cha Shirika la Habari Nchini, TBC1.

“Nawahakikishia wanahabari kwamba wako salama chini ya Serikali ya Awamu ya Tano na uongozi wa rais John Magufuli,” Nape alieleza.

Waziri Nape ameeleza kuwa serikali imeshirikiana na wadau wa habari na kutumia manoni yao kukamilisha muswada wa Sheria ya Habari ambao ameeleza kuwa utakuwa na manufaa makubwa kwa tasnia hiyo kwa ujumla utakapoanza kutumika kama sheria.

Nape aliwataka waandishi wa habari nchini kutumia fursa ya uhuru na ushirikiano wa serikali katika sekta hiyo, kuibua matatizo mbalimbali ya jamii ambayo yatatumiwa na serikali kama moja ya chanzo cha kuyabaini na kuyatatua.

Ne-Yo afunga ndoa na mrembo huyu
Jecha: Maalim Seif hakujitoa kushiriki uchaguzi wa marudio