Siku chache baada ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na baadhi ya vyama vya upinzani kueleza kuwa wameiandikia barua rasmi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuhusu kutoshiriki uchaguzi wa marudio, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jecha Salim Jecha amesisitiza kuwa hakuna aliyejitoa.

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha

Jecha aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa bado ofisi yake inawatambua wagombea wote walioshiriki uchaguzi wa Oktoba 25 kama wagombea wa uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu kwakuwa hakuna aliyejitoa kwa mujibu wa taratibu na sheria za uchaguzi.

“Mgombea urais wa CUF na wagombea wake wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na vyama vingine sita waliandika barua kwa ZEC wakisema hawatashiriki uchaguzi wa marudio. Kwa bahati mbaya, wagombea wote wa vyama vya siasa wameshindwa kufuata utaratibu na sheria ili kujitoa,” alisema Jecha.

Mwenyekiti huyo wa ZEC alieleza kuwa Kifungu cha 31 na 37 A na Sura ya 46 na 50 ya Sheria ya Uchaguzi  inaeleza wazi utaratibu wa kujitoa kwa mgombea, ambapo ni jukumu la Chama kuiandikia barua ZEC kuondoa udhamini wake kwa mgombea.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo, Tume hiyo imeendelea na maandalizi ya uchaguzi wa marudio na wagombea wote 14 wa nafasi za urais pamoja na wagombea wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani wataendelea kuorodhoshwa na kupigiwa kura.

Alieleza kuwa Tume hiyo inaendelea kukamilisha taratibu za kuwapatia ulinzi wa uhakika wagombea wote wa urais kwa saa 24 hadi matokeo yatakapotangazwa.

Nape atangaza Neema hii kwa waandishi wa habari
Watani wa Jadi: Mnyama Atafunwa