Kundi la Navy Kenzo linaundwa na Nahreel na Aika limesema kuwa liko tayari kuachia album yao mpya ya ‘Above in a minute’.

Kundi hilo limesema kuwa litaiachia album hiyo mapema mwaka 2016 lakini itauza album hiyo sio kwa kuimwaga sokoni bali watakaoitaka wataweka order mapema.

Album hiyo itauzwa online na kwenye CD na yeyote atajayeitaka atatakiwa kuweka order yake mapema.

“Hata kama ni online, unafanya order. Ukishalipia, siku ukitoka unapata yako. Baada ya hapo itakuwa ngumu, “alisema Nahreel ambaye ni mpishi wa album hiyo.

Album hiyo imewapa shavu R2Bees, Patoranking, Vee Money, Young Dee na Weusi.

Mkuu wa Mkoa Afuta Likizo za Watumishi Wote Mwaka Huu, Ataka Wachape Kazi Tu!
TRA wawacharukia wafanyabiashara, wapiga Makufuli Maduka