Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kuendana na Kasi ya ‘Hapa Kazi Tu’ na kutekeleza maagizo ya Rais John Magufuli aliyewataka kukusanya kodi.

Mamlaka hiyo imeanza kuchukua hatua kwa wafanyabiashara wote ambao hawatumii mashine za EFD na ambao hawana kabisa,  kwa kufunga maduka yao kwa Makufuli makubwa.

Zoezi hilo lilishuhudiwa jana katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo maafisa wa TRA walionekana wakibaini na kufunga maduka hayo.

Akiongea na waandishi wa habari, Afisa aliyekuwa anafanya kazi hiyo alieleza kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuwa wafanyabiashara hao wamekaidi amri na sheria halali na kwamba licha ya kuwatumia barua mara kadhaa hawakuzingatia.

Alisema zoezi hilo ni endelevu hivyo aliwasihi wafanyabiashara kuhakikisha wanatumia mashine za EFD.

 

 

 

Navy Kenzo Kuuza Album Yao Mpya Kipekee...
Mo Dewj ashinda tuzo ya Forbes, amshinda Rais wa Nigeria