Serikali imewatoa hofu wananchi wake kuwa nchi iko salama na itaendelea kuwa salama.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni, akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Tauhida Nyimbo (CCM) aliyetaka kauli ya serikali kutokana kuwapo kwa taarifa za vitisho zinazotolewa kwenye mtandao wakati huu wa maandalizi ya sikukuu ya Idd el Fitr.

Waziri Masauni alisema pamoja na kuwapo kwa vitendo vya kiuhalifu vinavyotokea, nchi bado iko salama na itaendelea kuwa salama kutokana na serikali kuhakikisha inadhibiti uhalifu huo.

Pia Serikali imesema mikutano ya kisiasa itaendelea kuzuiwa hadi pale polisi watakapoona inafaa kufanyika.

 

Mahakama Yapinga Uhamisho wa ''El Chapo''
Sarakasi Za Uongozi Wa Stand Utd Zaendelea