Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako amezitaka taasisi za dini kuziangalia shule zao ili ziwe na ada za kuridhisha ambazo haziwaumizi wazazi ili zifanane na huduma wanazotangaza.

Ameyasema hayo katika hotuba yake ya maadhimisho ya sherehe za miaka 25 ya Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) Jijini Dar es salaam, amesema kuwa baadhi ya shule hazifanani na maono ya hizo taasisi kama yanavyozungumziwa na juu ya kutoa huduma za Jamii.

“Baba Askofu Alex Malasusa, tuziangalie baadhi ya shule, kuna baadhi hazifanani na taasisi tunazoziongea, katika hali ya kawaida ili shule ipate usajili inatakiwa iwe na majengo, sasa unakuta hiyo michango ya majengo imekuwa endelevu kila mwaka mtoto analipishwa,”amesema Ndalichako.

Aidha, amesema kuwa kumekuwepo na malalamiko kuwa wanafunzi hawapangwi kwenye shule ama vyuo ambavyo wamevipa kipaumbele badala yake wanapangwa sehemu nyingine tofauti, ambapo amesema atalifanyia kazi suala hilo.

Kwa upande wake, Askofu Alex Malasusa ameiomba Serikali kufanyia kazi matatizo yanayoikabili Sekta ya elimu na taasisi za dini ili watoe huduma nzuri kwa jamii kama walivyokusudia.

Video: Lowassa, Warioba waibuka vita ya dawa za kulevya, Wanafunzi 8, 430 vyuo vikuu hawana sifa
Magazeti ya Tanzania leo Februari 23, 2017