Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amewataka wakurugenzi akiwamo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), wajipime iwapo utendaji wao unafaa kuendelea na nyadhifa walizonazo.

Ameyasema hayo alipokuwa akizindua bodi mpya ya Veta, amesema kuwa miradi mingi ya maendeleo imekwama pasipo na sababu zozote za  misingi.

Ndalichako amesema kuwa miradi hiyo yenye thamani ya sh 14.5 bilioni imekwama kutekelezwa, zikiwamo karakana 11 ambazo hazijajengwa, Nne zikiwa Mkoa wa Lindi, Manyara (4) na Pwani (3).

“Siridhishwi na utendaji wa Veta, watendaji wamekuwa watu wa michakato kila wakiulizwa wanasema mshauri elekezi hajapatikana, Vyuo vina mahitaji makubwa, kinacho nishangaza kumekuwa na kigugumizi katika ujenzi,”amesema Ndalichako.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Dkt. Bwire Ndazi amesema kuwa miradi hiyo ilikuwa inakwamishwa na utaratibu wa michakato ambayo imekuwa muda mrefu kutekelezeka.

Zlatan Ibrahimovic, Tyrone Mings Hatarini Kufungiwa
Magazeti ya Tanzania leo Machi 7, 2017