Chama cha soka nchini England FA kimewafungulia mashataka Mshambuliaji wa Man Utd Zlatan Ibrahimovic na Beki wa Bournemouth Tyrone Mings, baada ya kuonyesha mchezo mchafu wakati wa mpambano wa ligi kuu mwishoni mwa juma lililopita.

Wachezaji hao walionyeshana undava kwa kuchezeana faulo mara kwa mara wakati wa mchezo huo ambao ulishuhudia Man Utd wakilazimishwa sare ya bao moja kwa moja katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford.

Mings alionekana akimchezea faulo kwa kumkanyaga kichwani Ibrahimovic aliyekuwa ameanguka chini katika Dakika ya 44 na Dakika 2 baadae mshambuliaji huyo kutoka nchini Sweden alirudisha kwa kumpiga kiwiko.

Tokeo la picha la Zlatan Ibrahimovic and Tyrone Mings - sky sports

Wachezaji hao wamepewa muda hadi hii leo kujibu tuhuma zinazowakabili.

FA imefikia hatua ya kuwafungulia mashataka wawili hao, kutokana na makosa waliyofanya uwanjani kutoonwa na mwamuzi Kevin Friend, na yalinaswa kwenye picha za televisheni.

Kwa mujibu wa Kanuni za FA, Mchezaji kumpiga Kiwiko na Kumkanyaga mchezaji mwezake makusudi ni faulo ambazo zinastahili kutolewa kadi nyekundu na pia Kifungo cha kusimamishwa kucheza Michezo mitatu.

Ikiwa Wachezaji hao watapatikana na hatia, Ibrahimovic ataikosa Mchezo wa Robo Fainali ya FA CUP dhidi ya Chelsea na Mchezo wa Ligi dhidi ya Middlesbrough na West Bromwich Albion.

Kwa upande Mings, atakosa mchezo dhidi ya West Ham, Swansea City na Southampton.

Video: Aliyempa ardhi Makonda ahojiwa na Polisi, Lipumba awatumbua wakurugenzi 5 Z'bar
Ndalichako awataka wakurugenzi wa elimu kujitathmini