Ndege ya Shirika la Ndege la Precision, imepata ajali Bukoba na kuanguka katika Ziwa Victoria asubuhi ya leo Novemba 6, 2022.
Taarifa za awali, zinaonesha ndege hiyo imeanguka ziwani wakati ikijaribu kutua, uokoaji wa abiria unaendelea
Kwa mujibu wa mashuhuda, hali ya hewa ilikuwa mbaya huku kukiwa na mvua na ukungu uwanjani hapo, na usiache kufuatilia Dar24 Media kwa undani wa taarifa hizi ambazo zitakuijia hivi punde.