Watu wanne wamekufa ikiwa ni pamoja na mgonjwa wa moyo baada ya ndege maalum ya kubeba wagonjwa kuanguka katika eneo la maegesho ya magari, Nevada nchini Marekani saa chache zilizopita.

Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya ndege hiyo Piper PA31 kuruka katika uwanja wa ndege wa Elko. Wafanyakazi watatu wa ndege hiyo pamoja na mgonjwa huyo ndio waliofikwa na umauti.

Kwa mujibu wa New York Post, hakuna mtu yoyote aliyepapata madhara nje ya waliokuwa kwenye ndege hiyo iliyoanguka.

Mgonjwa aliyefariki alikuwa akikimbizwa katika hospitali iliyopo Chuo Kikuu cha Utah.

Kagera watakiwa kutobweteke na misaada ya tetemeko
Magufuli amtumbua Mwenyekiti wa Bodi ya TRA na Bodi yake