Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bernard Mchomvu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Rais Magufuli ameivunja pia Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka hiyo.

“Uteuzi wa Mwenyekiti mwingine wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA na Bodi ya Mamlaka hiyo utatangazwa baadae,” imeeleza taarifa hiyo.

Rais Magufuli ameendelea kupanga na kupangua safu ya watendaji wa Taasisi, Mamlaka na Mashirika ya Umma ili kufikia adhima yake ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Ndege yaanguka kwenye maegesho ya magari
Bashe adai Lowassa alionewa CCM, aeleza uhusiano wao kwa sasa