Ndege ndogo iliyobeba watu 21 imetoweka leo Ikiwa katika eneo la milima nchini Nepal wakati ikisafiri kutoka Pokhara kwenda Jomsom, eneo la mwanzo wa milima ya Himalaya.

“Abiria 18 pamoja na raia watatu wa nje ya nchi, na wafanyakazi watatu wa ndege hiyo walikuwa ndani ya ndege,” Msemaji wa Shirika la ndege la Tara, Bhim Raj Rai aliiambia AFP.

milima

Maafisa wa Nepal wameeleza kuwa huenda ndege hiyo iligonga sehemu ya milima hiyo baada ya kupoteza muelekeo.

Imeelezwa kuwa ndege hiyo ilitoweka baada ya kupoteza mawasiliano, dakika nane baada ya kuondoka katika mji wa magharibi ya Pokhara, Jumatano asubuhi.

Tayari timu ya uokoaji imeanza kufanya zoezi la utafutaji ikitumia helikopta katika eneo la milima hiyo.

Wenger aeleza ‘majuto’ yake baada ya kipigo cha Barcelona
‘CUF wanajiandaa Kushtukiza Uchaguzi wa Marudio Zanzibar’