Meneja wa Klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameeleza majuto yake akiwa na machungu ya kipigo cha nyumbani cha 2-0 walichopokea kutoka kwa klabu ya Hispania, Barcelona.

Babu Wenger ameeleza kuwa anajutia sana kupoteza nafasi za kwanza za kupachika magoli kabla hawajavurumishiwa kipigo na Barca, ambapo wachezaji wake Alex Oxlade na Olivier Giroud walikosa magoli ya wazi.

Olivier Giroud

Olivier Giroud

“Kitu nilichojutia ni kwamba mwanzo ilionekana kama tunatawala mchezo, tugawa magoli. Ni sawa na msimu uliopita kwa Monaco na hiyo inatuchanganya,” Kocha huyo wa washika Bunduki aliiambia BT Sport.

Wenger aliweka wazi pia kuwa anaipa Barca asilimia 95 ya kuingia katika hatua ya robo fainali katika mchezo wao wa marudiano ambapo wakati huu watakuwa na kibarua kizito zaidi wakiwa ugenini. Alisema kuwa ingawa wanalitambua hilo, wataenda kucheza.

Alisema kuwa hakuna sababu ya kuona aibu kusema ukweli kuwa Barcelona walikuwa wazuri zaidi yao katika mchezo huo.

Neymar na Lus Suarez walishirikiana kumtengenezea nafasi Lionel Messi kupachika goli la kwanza, na baadae kuongeza goli la penati lililoimaliza Arsenal, iliyotengwa na muamuzi baada ya Mathieu Flamini kumchezea madhambi ndani ya 18.

Usithubutu kwenda kwenye Usaili wa kazi bila kufahamu mambo haya manne
Ndege yapotea ikiwa na abiria 21