Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imepokea ujumbe wa Taasisi zaTume za Uchaguzi Duniani (AWEB) uliokuja kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya uendeshaji Uchaguzi.

Tume hiyo imekuja kujifunza kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) juu ya masuala mbalimbali ya uendeshaji Uchaguzi nchini ikiwemo matumizi ya vifaa vya kuandikishia wapiga kura.

Mkurugenzi wa Mipango na Oparesheni, Lee Ju-Hwan  alisema kuwa yeye na ujumbe wake wamekuja kubadilishana uzoefu katika technolojia ya Kuandikisha Wapiga Kura.

Ujumbe huo umekutana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani na kufanya mazungumzo naye ofisini kwake baada ya kukutana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya tume hiyo kutembelea ofisi mbalimbali za Tume hiyo na kujifunza.

Wakiwa katika kikao na baadhi ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na ujumbe huo wa watu watatu ulijifunza namna mashine ya Biometric Voter Registration (BVR) inavyofanya kazi na jinsi NEC ilivyoweza kuandikisha Wapiga Kura wengi kwa kutumia mashine technolojia hiyo  na changamoto zake.

Ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Mipango na Operesheni Lee Ju-Hwan, Mtafiti Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi Park Jae Sumg.

DC atishia kujiuzulu mbele ya Naibu Waziri
Video: Ziara ya JPM yaondoka na bosi Magereza, Sakata la Dangote lafichua siri nzito...