Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) leo Jumanne Julai 5, 2022 limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na kusema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 99.87.

Akitangaza matokeo hayo visiwani Zanzibar leo Kaimu Katibu wa Baraza Hilo, Athuman Amas amesema mwaka huu idadi ya ufaulu ni asilimia 99.87 ikilinganishwa na asilimia 99.62 ya mwaka jana.

Matokeo kidato cha sita 2022 haya hapa

“Watahiniwa 93,136, sawa na asilimia 98.97 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 40,907 sawa na wavulana waliofaulu ni 52, 229.

Ufaulu katika masomo ya Historia, Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Physics, Chemistry, Biology, Kilimo, Advanced Mathematics, Economics, Accountancy, na Food/HumanNutrition umepanda ikilinganishwa na mwaka 2021.

Hata hivyo, NECTA imesema ufaulu wa Masomo mengine yakiwemo General Studies, Geography na Basic Applied Mathematics (BAM) umeshuka.

https://matokeo.necta.go.tz/acsee2022/index.htm

Ummy Mwalimu:Barakoa bado lazima
Sakata la Arusha, Haji Manara aomba radhi hadharani