Shirikisho la soka duniani FIFA, limeipokonya point timu ya taifa ya Bolivia kupitia michezo yake ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Chile pamoja na Peru.

FIFA wametoa maamuzi ya kuipokonya point timu ya taifa hilo la kusini mwa Amerika, baada ya kujiridhisha mchezaji Nelson Cabrera alikosa sifa za kuitumikia Bolivia katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia, kwani aliwahi kuichezea timu ya Paraguay miaka kadhaa iliyopita.

Bolivia walikuwa wamejikusanyia point tatu kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa sifuri walioupata dhidi ya Peru na point moja iliyotokana na matokeo ya bila kufungana dhidi ya Chile mwezi uliopita.

Katika michezo hiyo miwili, mchezaji Nelson Cabrera alijumuishwa kwenye kikosi cha Bolivia, na kusababisha rapsha kwa wapinzani, jambo ambalo lilifanyiwa kazi kabla ya kukatiwa rufaa FIFA.

Kwa mantiki hiyo sasa, FIFA wametoa ushindi wa mabao matatu kwa sifuri kwa Peru pamoja na Chile dhidi ya Bolivia ambayo pia imetozwa faini ya Franga za Uswizi Elfu 12,000 sawa na Pauni Elfu10,000.

Maamuzi ya kupokonywa point nne, yanaifanya timu ya taifa ya Bolivia kushuka hadi katika nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo wa kundi la Amerika kusini.

Mara baada ya michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia katika ukanda wa Amerika ya kusini, timu nne za mwanzo katika msimamo wa kundi la ukanda huo zitakata tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ambazo zitafanyika nchini Urusi.

Mourinho Avishwa Kitanzi Kingine, Apewa Mpaka Ijumaa
Bunduki 11 za Ujangili zakutwa nyumbani kwa Mbunge