Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Brazili Neymar da Silva Santos Júnior, anatarajiwa kusaini mkataba mpya ambao utamuwezesha kuitumikia klabu ya FC Barcelona hadi mwezi Juni 2021.

Uongozi wa FC Barcelona na mshambuliaji huyo wanatarajiwa kumaliza suala hilo siku ya ijumaa.

Mkataba wa sasa wa Neymar unamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni 77,000 kwa juma hali ambayo ilizua tafrani miongoni mwa mashabiki wa soka duniani kwa kuhoji uwezo wake sambamba na na kiasi cha pesa anacholipwa.

Taarifa zinaeleza kuwa mkataba wa sasa wa Neymar utapandishiwa mshahara wake maradufu ambapo kwa mwaka atakua akipokea kiasi cha Euro 25,000,000 sawa na Pauni 435,000 kwa juma.

Kiasi hicho cha pesa kama mshahara wa Neymar, kitauzidi mshahara wa mshambuliaji na nahodha msaidizi wa FC Barcelona Lionel Messi ambaye anapokea kiasi cha Pauni 255,000 kwa juma huku Luis Suarez akipokea mshahara wa Pauni 200,000 kwa juma.

Neymar, alijiunga na FC Barcelona mwaka 2013 akitokea nchini kwao Brazil alipokua akiitumikia klabu ya Santos, na mpaka sasa ameshaifungia Barca mabao 31 katika michezo ya michuano yote aliyocheza.

Jose Mourinho Awakebehi Mashabiki Wa Liverpool
Jurgen Klopp: Tunapaswa Kujilaumu Wenyewe