Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ leo ijumaa (Februari 19) kinarusha karata yake ya pili kweye Fainali za Mataifa ya Afrika (U20 AFCON) dhidi ya Gambia.

‘Ngorongoro Heroes’ itashuka dimbani huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanz wa ‘Kundi C’ kwa kufunga nwa kikosi cha Ghana mabao manne kwa sifuri.

Kutokana na matokeo hayo ‘Ngorongoro Heroes’ italazimika kusaka ushindi kwa hali na mali mbele ya Gambia, ili kuendelea kuwa sehemu ya ushindani kwenye fainali hizo, kabla ya kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua inayofuata kwa kucheza dhidi ya Morocco.

Kocha Mkuu wa ‘Ngorongoro Heroes’ Jamuhuri Kiwelu Julio amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri na ana matumaini ya kufanya vyema katika mchezo wa leo dhidi ya Gambia.

“Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wetu wa leo, kwa hakika nimeyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ghana, sina budi kusema tupo katika mazingira mazuri ya kwenda kupambana,”

“Kikubwa watanzania waendelee kuwa pamoja na timu yao, watuombee dua ili tufanikishe azma ya ushindi kwenye mchezo wetu dhidi ya Gambia.” Amesema Julio.

Gambia ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Morocco kwa kufungwa bao moja kwa sifuri, nayo itakua na kila sababu za kuhitaji kuifunga Tanzania kwenye mchezo wa leo, ili kujihakikishia nafasi ya kuendelea kuwa sehemu ya fainali hizo.

‘TOTAL WAR, POINT OF NO RETURN’ kuimaliza Al Ahly Dar
Sakata la Morrison, Mwakalebela aitaja TFF