Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibu aliteua Wakuu wa Wilaya wapya 139, ambapo amewapa vijana kipaumbele na kuwapa nafasi ya kuwa viongozi katika serikali yake wasanii, waigizaji, wanamitindo na watangazaji hakuwacha nyuma katika uteuzi wake.

Katika mahojiano na kipindi cha The Plug cha Dar 24 media mtangazaji wa EFM Genisi Sanga amesema kuwa vijana walikuwa wanalalamika kuwa hawawekwi kwenye uongozi na rais Samia ameliona hilo na kuwapa nafasi sababu kizazi kinabadili na mambo yanabadilika.

”Kundi kubwa la watu ambao tuko hapa Tanzania ni vijana sasa unadeal nao vipi lazima uwape na wenyewe power ili wawaze kuwasaidia vijana wenzao , walete akili mpya viongozi wengi waliopo madarakani ni watu waliozaliwa miaka ya nyuma sana” amesema Sanga

Hii ndo suluhu ukatili dhidi ya watoto
Vita ya Marekani, Iran yapamba moto, vyombo vya Habari vyenye mfungamano na Iran vyafungiwa