Mwenyekiti wa Bodi ya Waadhamini ya NSSF, Balozi Ali Idi Siwa amewahakikishiwa wanachama wa NSSF kuwa Mfuko upo imara na kwamba una uwezo wa kuendelea kuwalipa Mafao mbalimbali kwa zaidi ya miaka 40 ijayo.

Balozi Siwa ameyasema hayo Julai 11, 2023 wakati alipotembelea Banda la NSSF katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa, “mfuko unaendelea kukua kwa kasi kubwa kwani hivi sasa ukwasi wa Mfuko umefikia thamani ya shilingi za kitanzania Trilioni 7.1 na kwamba NSSF inaendelea kuboresha mifumo ya ufanyaji kazi ili kuhakikisha kuwa huduma bora zinamfikia kila mwanachama.”

Hamsemi mazuri ya nchi, mnapotosha - Silaa
Kilimo cha Mirungi: Viongozi Halmashauri waonywa