Sio rahisi kufikiria kama Rais wa Marekani anaweza kulalamikia tatizo la kukosekana kwa mtandao ndani ya Ikulu ya nchi hiyo yenye nguvu na teknolojia kubwa duniani, lakini Obama ameweka wazi  kilio chake kabla hajaachia nafasi hiyo.

Akifanya mahojiano na Gayle King wa CBS, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi ya Super Bowl, Obama alieleza kuwa moja kati ya vitu vinavyomtatiza ndani ya Ikulu hiyo ni kukosekana kwa huduma ya Wi-Fi katika baadhi ya maeneo anayozungukia.

“Kuna maeneo mengi sana hayana wi-fi.. hili hunitatiza sana,” alisema Obama na kuongeza kuwa mabinti zake (Malia na Sasha) pia huchukizwa sana na hilo.

Hata hivyo, Rais Obama alieleza kuwa anapambana kuhakikisha kuwa analitatua tatizo hilo ili familia ya Rais ajae na jamaa zake wasikutane nalo.

Katika mahojiano hayo, Obama aliambatana na mkewe na mabinti zake wawili.

Angalia video mpya ya wimbo wa Beyonce 'Formation'
Angalia video mpya ya Wimbo wa Ali Kiba 'Lupela'