Mpango wa kubana matumizi unaoratibiwa kwa vitendo na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli umechukua sura mpya baada ya ofisi ya Waziri Mkuu kuonesha mfano usio kifani.

Ofisi hiyo nyeti ambayo chini yake kuna Wizara ya Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Walemavu itaanza kutumia usafiri wa pikipiki na bajaji unaotumia kiasi kidogo cha mafuta kuanzia Mwaka wa Fedha 2016/2017.

Mpango huo umebainika kupitia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoisoma jana Bungeni na kuungwa mkono na Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo, haikufafanuliwa zaidi ni watumishi wa ngazi gani watakaotumia usafiri huo katika kutekeleza majukumu yao.

 

Magufuli azungumzia kuhama kwa ‘Akina Lowassa’
Ukawa wasusia Bunge, washindilia misumari mitatu