Rais wa klabu ya Al Ittohad FC ya Misri Mohammed Mouselhy amesema hawafahamu alipo Mshambuliaji wao kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi.

Mouselhy amesema Mshambuliaji huyo ametoweka klabuni hapo bila kutoa taarifa, na kitendo hicho wanakichukulia kama utoro.

Kiongozi huyo amesema tayari wamuandikia barua ya kumpa onyo huku taarifa kutoka Uganda zinasema kuwa Okwi amemaliza mkataba na Klabu hiyo tangu June 30.

Okwi alijiunga na klabu hiyo mwaka 2019 akitokea kwa mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, lakini amekua na wakati mgumu wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza kwa kipindi kirefu.

Hivi karibuni Mshambuliaji huyo mwenye kismati na Ligi Kuu Tanzania Bara, alihusishwa na mpango wa kurejea Msimbazi yalipo makao makuu ya klabu ya Simba SC.

Simba SC ilipokwenda Cairo kwa ajili ya mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu kucheza dhidi ya Al Ahly, Okwi alionekana kuwa mwenye furaha alipowatembelea wachezaji wa klabu hiyo kambini kwao.

kitendo hicho kiliibua minong’ono iliyoanza kumuhusisha huenda akaonekana tena Simba SC msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa.

Ramos akamilisha PSG
Young Africans yalambwa Milioni 3