Klabu ya Young Africans imetozwa faini ya Shilingi Milioni tatu (3,000,000), baada ya kufanya makosa ya kikanuni wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba SC, uliochezwa Jumamosi (Julai 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo Young Africans walichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na kiungo Zawadi Mauya, dakika ya 12, na kuiwezesha klabu hiyo kuondoka na alama tatu muhimu dhidi ya Mabingwa watetezi Simba SC.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi Ligi Kuu Tanzania (TPLB), iliyokutana Julai 06, 2021 imejiridhishwa kuwa, Young Africans ilivunja kanuni za Ligi Kuu.

Makosa yaliyopelekea Young Africans kutozwa faini ya Shilingi milioni tatu (3,000,000), ni Kuitumia mageti ya Uwanja wa Uhuru kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya mlango maalum unaotumiwa na timu.

Kutumia mlango wa chumba cha waandishi wa habari (Media Center) badala ya mlango unaotumiwa na timu.

Kuingia uwanjani kupasha misuli mlango (Gate B) ambao haukupangwa kutumika kwa namna yoyote.

Kutumia chumba cha wafanya usafi wa uwanja kwa ajili ya kubadilishia nguo, badala ya chumba maalum cha kubadilishia nguo.

Sambamba na faini hiyo, pia Young Africans imetakiwa kulipa Shilingi 850,000 ikiwa ni gharama ya ukarabati wa mageti yaliyovunjwa wakati wakiiingia uwanjani pamoja na makufuli ya uwanja wa Benjamin Mkapa yaliyoharibiwa katika tukio hilo adhabu ambazo zimetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 15(15) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Okwi awakimbia waarabu
Young Africans yalamba dili zito