Mshambuliaji kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi, amemlaumu mwamizi Elii Sasii, kwa kushindwa kumlinda kutokana na rafu alizokuwa akichezewa na mabeki wa timu ya Yanga.

Okwi amesema mabeki wa Yanga, Kelvin Yondani na Endrew Vicent ‘Dante’, walistaili kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na rafu za mara kwa mara walizokuwa wakimchezea kwenye mchezo huo.

“Nilimlalamikia mwamuzi mara kwa mara kumtaka awe makini na wachezaji wale lakini chakushangaza mwamuzi aliendelea kuwaangalia na kushindwa kutoa hata kadi ya njano kwa mmoja wao jambo ambalo liliwapa uhuru wa kuendelea kucheza ndivyo sivyo,”amesema Okwi.

Mshambuliaji huyo mwenye mabao nane hadi sasa amesema kwa kiwango alichokuwa nacho hadhani kama Yanga wanauwezo wa kuizuia Simba pindi wanapotaka jambo lao na sare ya jana ilitokana na msaada kutoka kwa mwamuzi huyo.

Amesema alikuwa na hamu ya kuifunga Yanga, jana lakini baada ya jana kushindikana anaiweka hamu yake na kusubiri mchezo wa marudiano ambao utachezwa mwakani na kutamba kuwa atahakikisha anawafunga.

Azam FC wakiri moto wa Mbeya City Si wakuchezea
Majimaji FC wamuweka kando Abdulhalim Humud