Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, Christopher Ole Sendeka ametangaza nia ya kuwaanika baadhi ya viongozi wa vyama vya Upinzani ambao wamekuwa wakinufaika na ufisadi katika mafuta.

Ole Sendeka amesema kuwa baadhi ya viongozi hao ni wale ambao wamekuwa mstari wa mbele kutaka kupita kila mkoa wakidai wanaishtaki Serikali kwa wananchi.

Hivi karibuni, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilitangaza kuanza operesheni ya kuishitaki Serikali kwa wananchi kwa kile wanachodai kuikandamiza demokrasia na utumbuaji majipu usiofuata sheria na taratibu.

Ole Sendeka alisema kuwa baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakifaidika na ufisadi ambao umetokana na vinasaba vinavyowekwa katika mafuta ingawa majina yao hayakutumika moja kwa moja.

Alisema kuwa watu hao ndio wako msitari wa mbele kukosoa utumbuaji majipu kwani umewaathiri katika ‘dili’ lao.

Kama ilivyokuwa kwa ‘list of shame’ iliyotolewa na Chadema miaka kadhaa iliyopita, Ole Sendeka ameahidi kuja na orodha itakayoyaanika hadharani majina yote ya watu hao na namna walivyokuwa wakinufaika.

“Siku ikifika orodha inaelekea kukamilika na nitaanika jina la kila mmoja baada ya mwingine. Ngoja nikamilishe taarifa maana ipo ambayo haijajitosheleza,” alisema.

“Ikikamilka nitataja mmoja baada ya mwingine na manufaa ambayo alikuwa akiyapata kuanzia huko kwenye vina saba,” aliongeza.

Kabla ya kupigwa marufuku kwa mikutano yote ya hadhara ya kisiasa nchini, CCM waliahidi kupita kila sehemu ambayo Chadema watapita kwa lengo la kusafisha hewa na kuwaeleza wananchi ukweli.

Video: Mbowe akamatwa, Zitto asakwa. Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bil. 2
Baada ya kuikimbia Chadema, Ole Medeye atoa msimamo wake kuhusu Lowassa