Mabao ya washambuliaji Hal Robson-Kanu (West Brom, Wales), Lionel Messi (FC Barcelona, Argentina) pamoja na Neymar (Fc Barcelona, Brazil) yameingia katika ushindani wa kuwania tuzo ya goli bora la mwaka 2016 (Puskas Award).

Robson-Kanu ameingai katika orodha ya wachezaji 10 bora kufuatia bao lake alilolifunga kwa umahiri mkubwa wakati wa fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2016) dhidi ya Ubelgiji.

Mshambuliaji huyo alifunga bao hilo katika mchezo wa robo fainali, ambapo aliwahadaa mabeki wa Ubelgiji katika eneo la hatari na kufanikiwa kuukwamisha mpira wavuni katika kona ya lango na wapinzani.

Bao la Messi lililotokana na adhabu ndogo dhidi ya Marekani katika michuano ya Copa Amerika limemuwezesha kuingia katika orodha hiyo huku Neymar akiingia kupitia bao maridadi alilolifunga dhidi ya Villarreal.

Orodha ya wachezaji wengine waliopo kwenye kinyanganyiro cha kuwania tuzo ya bao bora la mwaka 2016 ni Mario Gaspar (Spain), Hlompho Kekana (South Africa), Marlone (Brazil), Lionel Messi (Argentina), Neymar (Brazil), Saul Niguez (Spain), Hal Robson-Kanu (Wales), Daniuska Rodriguez (Venezuela), Simon Skrabb (Finland) na Mohd Faiz Subri (Malaysia).

1. Lionel Messi (Argentina)

2. Hal Robson-Kanu (Wales)

 3 Mohd Faiz Subri (Malaysia)

4. Neymar (Brazil)

5. Saul Niguez (Spain)

6. Mario Gaspar (Spain)

7. Simon Skrabb (Finland)

8. Hlompho Kekana (South Africa)

9. Marlone (Brazil)

10. Daniuska Rodriguez (Venezuela)

Lowassa, Sumaye waizawadia Chadema Mkakati wa CCM
40 Kuunda Kikosi Bora Cha Mwaka 2016