Baada ya mgogoro mkubwa ulioivunja P-Square na kupelekea kila mmoja kuanza kutangaza kufanya kazi zake binafsi, Paul amejishusha na kumbembeleza ndugu yake warudishe kundi lao kama familia.

Kupitia Instagram, Paul ameandika ujumbe mrefu akimuomba ndugu yake kutokubali kugawanywa na ushabiki wa mitandao ya kijamii na kumuomba amsamehe pale walipotereza.

Paul alijiuliza maswali matatu ambayo mojawapo lilikuwa kuhusu binamu yao ‘Jude Okoye’ ambaye alionekana kuwa moja kati ya sababu za ugomvi wao baada ya Peter kumtaka ajiondoe kuwa meneja. Paul alihoji kuwa hata baada ya Jude kuacha kusimamia kazi zao kwa kipindi cha mwezi mmoja bado wameendelea kugombana?

Paul ambaye anadaiwa kuwa mwandishi wa nyimbo nyingi zaidi za P-Square alikemea tabia ya kuanzishwa kwa timu za kuwagawanya kwenye mitandao ya kijamii pamoja na promota ambao wameanza kujitokeza kuomba shows za mmoja mmoja.

pls nobody shld support any teamPaul sh*t, I don’t need that.. Pls resist from it cos thats evil…and for those of you promoters ,supporting him to be performing psquare’s songs alone on stage, you are only killing us and destroying us the more,” aliandika Paul.

Alimuomba ndugu yake warudisha familia yao pamoja kwani watu wengi sio tu kwamba wanapenda muziki mzuri wanaofanya lakini pia wanapenda kuwaona wao kama ndugu wakifanya kazi pamoja.

Dear brother am begging you ,even if you don’t want Jude anymore and you don’t want psquare, u re forever going to be my brother … But I wish the 3 of us could still do these together, bcos its a thing of joy….people love us so much not only because of our good music but seeing brothers doing it together and keeping it together, setting a good example to other families and to our kids.Pls swallow ur pride, forgive and forget, we can still turn these things around…. If I have said anything or done anything that hurts you. Am very sorry…. And to all our true fans pls pray for us. God bless you all.

Siku moja baada ya maandishi hayo, inaonekana mapacha hao walirudi pamoja na kulirudisha kundi lao kwani walianza kupost tangazo la show yao ya pamoja ya Machi 26 nchini Uholanzi.

P Square

Makonda adai hata akifa ameshafanikiwa, atangaza vita kali na wauza Unga
Ndege kubwa yaanguka na kuua makumi