Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis anatarajia kufanya ziara mwanzoni katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na Sudan Kusini (Januari 31 hadi Februari 3, 2023).
Awali, ziara ya Papa Francis iliahirishwa kutokana na matatizo ya goti, ambapo sasa itafanyika katika muda huo huku akitarajia kuutembelea mji wa Kinshasa, akiambatana na Askofu Mkuu wa Canterbury na Msimamizi wa Baraza Kuu la Kanisa la Scotland.
Aidha, Papa Francis atafanya pia ziara ya amani katika mji wa Juba, huko Sudan Kusini, kuanzia Februari 3 hadi 5 mwakani.
Julai, 2022 Papa Francis alisema kuwa mkristo daima huleta amani kwa kuzingatia mada ya maridhiano aliyoipanga kuipatia kipaumbele katika ziara yake barani Afrika.