Papa Francis anahitimisha hija yake nchini Sudan Kusini kwa misa ya wazi Jumapili baada ya kuwataka viongozi wake kuzingatia kuleta amani katika nchi hiyo tete iliyosambaratishwa na ghasia na umaskini.
Safari hiyo ya siku tatu ni ziara ya kwanza ya Papa katika nchi hiyo yenye Wakristo wengi tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka 2011 na kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe iliyoua karibu watu 400,000.
Licha ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwaka wa 2018 kati ya Rais Salva Kiir na naibu wake Riek Machar, ghasia zinaendelea kulikumba taifa hilo jipya zaidi duniani, na kuwafukuza watu kutoka makwao hadi kwenye kambi za wakimbizi.
Papa, amekaribishwa kwa furaha, huku maelfu wakitarajiwa kuhudhuria misa hiyo katika kaburi la John Garang lililojengwa kwa heshima ya shujaa wa waasi wa Sudan Kusini aliyefariki mwaka 2005.
Papa Francis alikutana na wahanga wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambao waliletwa katika mji mkuu Juba kutoka kambi mbalimbali, na kuitaka serikali kurejesha heshima kwa mamilioni walioathiriwa na migogoro.
“Kwa kusikitisha, katika nchi hii iliyokumbwa na vita, kuwa mtu aliyehamishwa au mkimbizi imekuwa jambo la kawaida na la pamoja,” alisema.
“Nataka kufufua ombi langu la nguvu na la dhati la kumaliza migogoro yote na kuanza tena mchakato wa amani kwa umakini, ili ghasia ziweze kukomeshwa na watu warudi kuishi kwa heshima.”
Ikiwa na wakimbizi wa ndani milioni 2.2 (IDPs), na wengine milioni mbili nje ya nchi, Sudan Kusini ndiyo nyumbani kwa mzozo mbaya zaidi wa wakimbizi barani Afrika.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP John Wiyual mwenye umri wa miaka 42 , ambaye ameishi katika kambi kubwa ya IDP nje ya Juba tangu 2014 aliliambia shirika hilo kuwa “Wanasema kuna amani lakini kuna mauaji katika majimbo yote, Papa anaweza kutusikiliza. Sisi ni raia, na tunahitaji amani.”
Ziara ya Papa imefuatiliwa kwa karibu katika nchi hiyo yenye watu milioni 12, ambapo viongozi wa makanisa walichukua jukumu muhimu katika kuwalinda raia wakati wa harakati za kudai uhuru na mzozo wa kikabila wa 2013-18.
Takriban watu 50,000 walimiminika kwenye kaburi la Garang Jumamosi jioni kwa ajili ya mkutano wa maombi wa pamoja uliofanywa na Francis pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury na Msimamizi wa Baraza Kuu la Kanisa la Scotland, ambao pia ni sehemu ya safari hiyo.
Papa Francis, aliwaambia viongozi wa nchi hiyo kwamba wanahitaji kufanya mwanzo mpya kuelekea maridhiano na kumaliza uroho na vita vya kugombea madaraka vinavyosambaratisha taifa.
“Vizazi vijavyo vitaheshimu majina yako au kufuta kumbukumbu zao, kulingana na kile unachofanya sasa,” aliiambia hadhira iliyojumuisha Kiir na Machar, pamoja na wanadiplomasia, viongozi wa kidini na wafalme wa jadi.
“Hakuna umwagaji wa damu tena, hakuna migogoro tena, hakuna vurugu tena.”
Katika matukio ambayo yalijiri nchini Sudan Kusini, Francis alipiga magoti na kumbusu miguu ya maadui wawili ambao majeshi yao ya kibinafsi yameshutumiwa kwa uhalifu wa kutisha wa kivita.
Lakini miaka minne baadaye, nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta imesalia katika migogoro isiyoweza kutatulika na kuathiriwa na umaskini, njaa na majanga ya asili.
Kamanda wa waasi aliyesifiwa sana, Garang alikuwa rais wa kwanza wa Sudan Kusini iliyokuwa na uhuru nusu wakati kifo chake katika ajali ya helikopta mwaka 2005 kilifungua njia kwa naibu wake Kiir kuchukua hatamu.
Kusimama kwa papa nchini Sudan Kusini kunafuatia ziara ya siku nne katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nchi nyingine yenye rasilimali nyingi inayokumbwa na migogoro inayoendelea na ambayo mara nyingi hupuuzwa na ulimwengu.