Aliyewahi Kuwa Kocha Mkuu Simba SC Patrick Aussems amezua taharuki katika Vyombo vya Habari nchini Kenya na Rwanda, kufuatia kukanusha taarifa za kuihama klabu ya AFC Leopard.

Juma lililopita Aussems aliripotiwa kutimkia Rwanda kujiunga na klabu ya Kyovu FC, na alitarajiwa kutambulishwa rasmi kama Kocha Mkuu wa klabu hiyo siku kadhaa zijazo.

Uongozi wa AFC Leopard umesisitiza kumtambua Kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji kama Kocha wao Mkuu, na wanamsubiri nchini Kenya kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo.

Mwenyekiti wa AFC Leopards Dan Shikanda na Kocha Msaidizi Tom Juma wamesema kwa pamoja kuwa, Aussems bado ni Kocha Mkuu wa klabu hiyo na hawadhani kama taarifa za kuhamia Kyovu FC zilizokua sahihi.

Shikanda amesema klabu yake haijapata taarifa rasmi ya kiofisi juu ya kuondoka kwa Aussems.
Mwenyewe Aussems kupitia ukurasa wake wa twitter amekanusha kujiunga na Kiyovu na kuandika: “All these rumors I am quiet at home… Let me enjoy my holidays. Good evening everyone!”

Akimaanisha: “Hizo ni tetesi, mimi nimetulia tuli nyumbani, acha nifurahie mapumziko yangu, muwe na jioni njema”

Viongozi wa dini 'chachu' kasi ya chanjo Uviko-19
Singida Big Stars yawaita Polisi Tanzania