Uongzoi wa Singida Big Stars umewaita mezani Viongozi wa Polisi Tanzania ili kumaliza mzozo wa usajili wa Mlinda Lango Metacha Mnata unaoendelea kwa sasa.

Metacha Mnata alitambulishwa kuwa mchezaji wa Singida Big Stars mwanzoni mwa juma hili, huku Uongozi wa Polisi Tanzania ukidai unaendelesa kumtambua kama mchezaji wao halali kwa mujibu wa mkataba.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Singida Big Stars, Muhibu Kanu amesema wapo tayari kuzungumza na Viongozi wa Polisi Tanzania ili kumaliza mzozo huo, ambao unaendelea kuchukua nafasi kubwa katika medani ya Soka la Bongo.

Amesema Singida Big Stars ilijiridhisha kabla ya kuingia mkataba wa miaka miwili na Mlinda Lango huyo, hivyo ina ushahidi ambao unadhihirisha Metacha alikua huru.

“Kama kuna lolote ambalo ni tofauti na hili ambalo tunaliamini sisi, tunawakaribisha viongozi wa Polisi Tanzania waje tuzungumze, kwa sababu kuna tatizo hapa, hatuna budi kulimaliza kwanza, kwa sababu tunahitaji kuanza msimu tukiwa safi.”

“Haitapendeza kuanza msimu mkawa na maneno na upande mwingine, Metacha amesajiliwa Singida Big Stars kwa mkataba wa miaka miwili, hivyo kama kuna tatizo lolote wenzetu wanakaribishwa mezani ili kumaliza huu mzozo, ambao naona unaendelea kushika kasi kubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.” amesema Muhibu Kanu

Metacha Mnata alisajiliwa Polisi Tanzania mwanzoni mwa msimu uliopita 2021/22, baada ya kuachana na Young Africans mwishoni mwa msimu wa 2020/21.

Patrick Aussems achafua hali ya hewa Kenya, Rwanda
Geita Gold FC yapewa ruhusa kusajili 2022/23