Kiungo wa Man Utd Paul Pogba amerejesha vijembe kwa wadau wa soka waliokua wakichonga dhidi yake kufuatia mambo kutomnyookea tangu alipotua Old Trafford miezi miwili iliyoopita.

Pogba amerusha vijembe vya maneno baada ya kuwika katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya Uholanzi, uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo na kufanikiwa kufunga bao pakee ambalo liliipa ushindi timu yake ya taifa ya Ufaransa.

Pogba amesema siku zote hakua nafasi ya kusikiliza nini kinachozungumzwa dhidi yake na watu ambao hawakuonyesha kumkubali tangu alipotua Man Utd, na badala yake alifanya jitihada za kuhakikisha anaerejesha makali yake anapokua uwanjani.

Amesema ilimchukua muda kupisha maneno ya watu hao kuzungumzwa na kuandikwa katika vyombo vya habari, lakini bado alitambua lengo lake ni kucheza soka na alijua utafika wakati wa kulimaliza tatizo hilo kwa vitendo.

Katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo, Pogba alifunga bao la ushindi kwa Ufaransa kufuatia shuti kali ambalo lilielekea moja kwa moja langoni mwa Uholanzi ambao walikua nyumbani mjini Amsterdam.

“Ninafurahishwa na ushindi tulioupata na sina budi kuwashukuru wenzangu ambao tumeshirikiana nao katika mpango huu, lakini naamini itakua ni mbaya zaidi kwa wale waliokua wanazungumza kuhusu uwezo wangu wa kucheza soka tangu nilipoihama Juventus na kurejea Man Utd,”

“Ilinilazimu kucheza kwa juhudi na maarifa kutokana na mchezo huu kuwa na uzito mkubwa hasa ukingatia Uholanzi wana historia nzuri hali kadhalika na sisi Ufaransa ni hivyo hivyo.

“Naamini mambo yatakaa sawa muda si mrefu na daima sitozungumza kwa lengo la kumjibu mtu ambaye alizungumza sana kuhusu mimi, bali nitahakikisha vitendo vinakuwa vingi zaidi ili kuonyesha nini maana ya mchezo wa soka.”Alisema Pogba

Anthony Taylor Kuchezesha Liverpool Vs Man Utd
Wayne Rooney: Bado Nina Nafasi Ya Kurejesha Makali