Meneja wa Man City Pep Guardiola huenda akabadili msimamo wake na kusaini mkataba mpya pindi mkataba wake wa sasa utakapofikia kikomo mwaka 2019.

Guardiola anatarajiwa kufanya maamuzi tofauti, baada ya kukutana na mmiliki wa klabu ya Man City Sheikh Mansour huko Abu Dhabi juma lililopita na kufanya kikao kilichochukua saa kadhaa.

Guardiola alikutana na bosi wake kwa mara ya kwanza tangu alipokubali kusaini mkataba wa kukinoa kikosi cha Man City mwaka jana, na jambo kubwa ambalo linatajwa kuzungumzwa katika kikao hicho ni kuhusu mustakabali wake.

Katika kikao hicho mwenyekiti wa klabu ya Man City Khaldoon Al Mubarak alishiriki na kuchangia baadhi ya mambo ambayo yametumika kama ushawishi kwa meneja huyo kutoka nchini Hispania.

Guardiola amezungumzia kwa uchache suala la kikao hicho kilichofanyika mashariki ya kati kwa kusema, ilikua bahati kubwa kukutana na Sheikh Mansour na wamezungumza mambo mengi ya kimaendelea kuhusu Man City.

Hata hivyo hakutaka kuweka wazi nini matarajio yake baada ya kufanya mazungumzo na tajiri huyo, lakini akasisitiza suala la kuendelea kufanya kazi klabuni hapo kwa misingi ya makubaliano iliopo.

Guardiola aliwahi kusema hana mpango wa kusaini mkataba mpya, na ataondoka Etihad Stadium mara baada ya mkataba wake wa sasa kufikia kikomo mwaka 2019.

Guardiola alikabidhiwa kikosi cha Man City mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kutimuliwa kwa Manuel Pellegrini.

Nape: Nitahakikisha Timu Za Dodoma Zinacheza Ligi Kuu
Serge Gnabry Awindwa Allianz Arena