Safari ya Real Madrid ilikuwa ni safari ngumu iliyojaa misukosuko kama safari ya Wana wa Israel kuondoka Katika nchi ya utumwa kuelekea nchi ya ahadi yaani kaanani iliyoongozwa na nabii Mussa lakini safari ya Real Madrid 2022 Katika michuano ya Uefa Champions League imeongozwa na dereve mahiri, Nahodha shujaa na Rubani mwenye Maarifa na Anga Carlo Ancelot.

Wakati Daudi anakubali kwenda vitani kupambana na Goliati Carlo Ancelot yeye alikubali kukabiliana na changamoto zote kuanzia hatua ya makundi walipotupwa kundi D wakiwakuta Inter Milan, FC Sheriff pamoja na Shakhtar Donetsk lakini walivuka kwa Alama 15.

Wakiwa Katika kundi hilo wamemaliza vinara wa wakifuatiwa na inter milan Alama 10, F CSheriff Alama 7 na Shakhtar Donetsk Alama 2 pekee na walifanikiwa kufunga magoli 14 Katika michezo yao 6 wakifunga magoli 3 na kupoteza mchezo 1 pekee dhidi ya FC Sheriff.

PSG yenye Klyan Mbappe ilimrudisha darasani mwalimu Carlo Ancelot baada ya Droo iliyotolewa na kuwakutanisha hatua ya 16 bora nyuso za wafaransa na mashabiki wa Madrid zilijaa matumaini baada ya ushindi wa goli 1-0 Katika mchezo wa kwanza hawakujua maana ya ya msemo wa waswali kuwa “HAIJAISHA HADI IISHE”.

Mchezo wa pili nikasikia Sauti nyororo na nzito zaidi zikiimba “Halaaa Madrid” shujaa Karim Benzema alipopiga Hat Trick na Madrid anashinda 3-1 na kuwasaidia Real Madrid kuvuka kwa jumla ya goli 3-2.

Kituo kilichofuata ni mitaa ya The Blues ikiwa ni hatua ya Robo Final halloo Karim Benzema kwa Hat Trick nyingine pale daraja vita iliyoisha kwa Madrid kushinda 3-1 lakini kitabu cha Luka Mtakatifu 19:26 imeandika kuwa “Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho”.

Mchezo wa mkondo wa pili maandiko yanatimia licha ya Chelsea kutaka kupindua meza lakini kilichonenwa Katika maandiko hakipingiki licha ya kichapo cha goli 3-2 madrid anavuka kwa jumla ya goli 5-4.

Waswahili husema mwisho wa safari Moja ni mwanzo wa safari nyingine miamba ya nchini hispania ilibisha hodi kutoka mitaa ya darajani Hadi jiji la Machester kuleee mitaa ya Etihad Stadium kwenda kuwakabili mabingwa wa EPL msimu wa 2022 ikiwa ni hatua ya Nusu Finali.

Je, unakumbuka kile kicheko alichocheka Pep Gardiola kilimaanisha nini baada ya ushindi wa goli 4-3 kilichomfanya Carlo Ancelot akiwaze kwa week Moja ?

Duuuuuh kweli nimeamini kila Jambo na wakati wake wakati wa kucheka na wakati wa kulia kwani mchezo wa pili kijana mdogo asiye na ndevu jina lake linaanzia na R ila sio Rehema, Ramadhani wala Rahma ila ni Rodrigo aliyeingia kutoka Sub na kuwasaidia madrid kushinda 3-1 baada ya kufunga magoli 2 wakavuka tena KWA goli 6-5.

Hakutamani kuchagua kituo kingine kwa kutumia bali walitamani kuvuka Maji lakini nauli yao haikutosha kujenga makao walipokuwa na kuwafanya kubisha hodi pale pale kwao na Boris Johnson ambaye ni waziri mkuu wa uingereza ila wakachagua mtaa mwingine yaani mitaa ya Anfield ikiwa ni hatua ya Finali.

Kabla ya mchezo huo nikasikia Sauti nyingi masikini mwangu mara ” You will never walk alone” lakini kwa mbali nasikia ” Halaaa Madrid ” na Alama Moja ya moto nikastaajabu bila kujua.

Baadae nikapokea ujumbe kuwa ni fainal ya UEFA Champions League wanaume hao watakutana tarehe 28 may 2022 ila sio Anfield wala Santiago Bernabeu lakini itakuwa kule Paris nchini ufaransa ila mimi nilikosa tiketi tu kuelekea kule nikaishia zangu kukeketi na wadau kibanda umiza.

Nilikaza macho kutazama kilichoonekana kwenye TV mara nikasikia kelele na Sauti za kitanzania Yeeeeeeeeh kumbe ni Vin Junior.

Nilimuuliza jirani yangu wa kushoto aliyekuwa anakunywa zake soda ya barida Vin kafanya nini bro akacheka kwa Sauti kubwa baadae alinijibu tu kuwa kaweka kamba kalikumbe ni goli pekee lililowapa ubingwa vijana wa Carlo Ancelot Real Madrid.

Ukiumia wewe kuna mtu anafaidika kupitia kilio chako na jasho lako vijana wa Klopp wamelia kuukosa Ubingwa waluouhitaji Sana akilini mwao lakini Hongereni sana Real Madrid kwa ubingwa wenu hakika mmeonyesha ukongwe wenu Katika mashindano ya Uefa Champions ila Liverpool mmeonyesha kuwa mnajua kucheza mpira Katika hatua zote mimi huyooooooooo narudi zangu Tanzania elimu nilivyoipata yatosha nitarudi ulaya kuongeza masters Hadi PhD.

By Elishaaa Petro “Jr “

Mganga mkuu Wilaya ya Kigoma kuondolewa
Tanzania yapendekeza mkakati wa pamoja kupambana na ugaidi