Mabingwa wa Ligi Kuu England Liverpool usiku wa kuamkia leo Julai 23, 2020 walikabidhiwa kombe lao baada ya kugawa dozi ya mabao matano kwa matatu dhidi ya Chelsea.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Naby Keita, Alexander Arnold, Wijnaldum, Roberto Firmino na Chamberlin.

Kwa upande wa Chelsea mabao yalifungwa na Olivier Giroud, Tammy Abraham na Pulisic.

Machester United wamepanda hadi nafasi ya tatu baada ya kulazimisha sare ya moja kw amoja dhidi ya wagonga nyundo wa London West Ham na kufikisha alama 63.

Timu zote zimebakisha mchezo mmoja kumaliza Ligi hiyo msimu huu 2019/20 ambayo ilisimama kwa muda baada ya kuwepo ugonjwa wa Corona uliozikumba nchi mbalimbali duniani.

Wavuvi Kigamboni walia na kanuni mpya
Coastal Union kufuta unyonge kwa Simba SC leo?